Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 02:58

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani yupo ziarani barani Afrika


Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.
Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

Blinken atatembelea Porto da Praia iliyopokea ufadhili  kwa ajili ya juhudi za kisasa kutoka kwa Shirika la Millenium Challenge la serikali ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, anatarajiwa kukutana Jumatatu na Waziri Mkuu wa Cape Verde Ulisses Correia e Silva, wakati mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Marekani akianza ziara ya mataifa manne barani Afrika.

Ziara ya Blinken pia inajumuisha ziara ya Porto da Praia, ambayo ilipokea ufadhili kwa ajili ya juhudi za kisasa kutoka kwa Shirika la Millenium Challenge la serikali ya Marekani, na kuhudhuria mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika, kati ya Ivory Coast na Equatorial Guinea.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, amesema kabla ya ziara hiyo kwamba Blinken atasisitiza uwekezaji wa miundombinu ya Marekani barani Afrika kama njia ya “kuimarisha biashara ya pande mbili, kufungua nafasi za ajira nyumbani na kwenye bara hilo, na kuisaidia Afrika kushindana katika soko la kimataifa.

Molly Phee, waziri mdogo wa mambo ya nje wa masuala ya Afrika, aliisifu Cape Verde kabla ya ziara ya Blinken, akiitaja nchi hiyo kuwa na “demokrasia nzuri”. Ziara ya Blinken pia inajumuisha kuzitembelea Ivory Coast, Nigeria, na Angola.

Forum

XS
SM
MD
LG