Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 18:43

Desantis asitisha kampeni yake kuwania urais, amuidhinisha Trump


Gavana wa Florida Ron DeSantis alipotangaza kwamba anajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Gavana wa Florida Ron DeSantis alipotangaza kwamba anajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Gavana wa Florida Ron DeSantis Jumapili alisimamisha kampeni zake za kuwania urais kupitia chama cha Republican na kumuidhinisha rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, siku mbili kabla ya uchaguzi wa mchujo katika jimbo la New Hampshire.

Hatua hiyo inafikisha kikomo azma ya Desantis ya kuingia White House baada ya kushindwa kukidhi vigezo ambavyo vingemfanya mpinzani mkubwa zaidi wa rais huyo wa zamani.

"Ni wazi kwangu kwamba wapiga kura wengi wa mchujo wa chama cha Republican wanataka kumpa Donald Trump nafasi nyingine," alisema katika hotuba aliyoitoa katika jimbo la New Hampshire, ujumbe sawa na alioutoa awali kupitia mtandao wa X.

DeSantis alimdhihaki Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley, ambaye kwa muda mrefu alikuwa mpinzani wake wa karibu kwa nafasi ya pili katika kinyang'anyiro cha kutafuta tikiti ya chama hicho, akisema kwamba "hafai kuwa rais wa Marekani."

Gavana huyo, ambaye amekuwa akionyesha shauku kubwa, aliingia kwenye kinyang'anyiro cha urais wa 2024 akiwa na matumaini makubwa katika azma yake ya kumshinda Trump, na kura za maoni za awali zilionyesha kwamba alikuwa katika nafasi nzuri ya kufanya hivyo.

Yeye na washirika wake walichangisha zaidi ya dola milioni 100, na alijivunia rekodi yake ya kisheria kuhusu masuala muhimu kwa wahafidhina wengi, kama vile utoaji mimba na mafunzo ya masuala ya rangi na jinsia shuleni.

Wiki jana, alishindwa uchaguzi wa mchujo katika jimbo la Iowa - ambao alikuwa ameapa kushinda - kwa asilimia 30 kwa Trump.

Hatua ya Desantis ya kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho sasa inawaacha Trump na gavana wa zamani wa jimbo la South Carolina kushindania nafasi hiyo, siku moja kabla ya uchaguzi wa awali wa chama hicho katika jimbo la New Hampshire.

Forum

XS
SM
MD
LG