Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 13:53

Trump ashinda uchaguzi wa awali wa kumpata mgombea, aweka rikodi


Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

“ Huu umekuwa uzeofu wa kipekee. Wananchi wamekuwa... hii ni mara ya tatu tunashinda . lakini hii ndiyo kubwa zaidi.”

Rais wa zamani wa Marekani ameshinda katika uchaguzi wa awali na kuweka rekodi dhidi ya mpinzani wake wa karibu Gavana wa Florida Ron DeSantis.

Kwa upande wake De Santis alimshinda balozi wa zamani wa umoja wa mataifa Nikki Haley baada ya ushindani mkali .

Wote wawili walikuwa wakilenga kumaliza kwa nguvu katika nafasi ya pili ili kuwaonyesha wapiga kura na wafadhili kwamba changamoto zao bado zipo dhidi ya Trump.

Huku asilimia 95 ya kura zikiwa zimehesabiwa , Trump alikuwa na asilimia 51 , DeSantis asilimia 21 na Haley asilimia 19 , kulingana na utafiti wa kura wa Edison.

Kwa mujibu wa utafiti huo , theluthi mbili ya watu walioshiriki katika uchaguzi huo wa awali bado wanadhani Trump anafaa kuwa rais wa Marekani hata kama atakutwa na hatia ya uhalifu.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG