Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 02:59

Hali ya hewa ya baridi kali na theluji inatishia kusitisha shughuli Marekani


Hali ya hewa inavyoonekana katika jimbo la Iowa nchini Marekani
Hali ya hewa inavyoonekana katika jimbo la Iowa nchini Marekani

Idara ya hali ya hewa ya taifa imesema upepo unatarajiwa kusukuma baridi katika nyuzi joto 34 chini ya sifuri Celsius

Mlipuko hatari wa Arctic utaendelea kusambaa kote Marekani siku ya Jumatatu na kuendelea angalau mpaka katikati ya wiki, na kuongeza muda wa baridi kali ambayo inaweka rekodi ya chini ya baridi katika sehemu za nchi na kutishia kuvuruga zaidi maisha ya kila siku, ikijumuisha mchezo wa Football wa Marekani (NFL) na kinyang’anyiro cha kwanza cha uteuzi wa rais kwenye jimbo la Iowa.

Idara ya hali ya hewa ya taifa imesema upepo unatarajiwa kusukuma baridi katika nyuzi joto 34 chini ya sifuri Celsius, kutoka Northern Rockies kuelekea kaskazini mwa Kansas na kuingia Iowa, na kutoa changamoto kwa wapiga kura walio tayari kukabiliana na baridi kali leo Jumatatu.

“Huwezi kukaa nyumbani,” rais wa zamani Donald Trump aliwaambia wafuasi wake siku ya Jumapili. Dhoruba za Arctic zilisababisha vifo vya angalau watu wanne na kukata umeme kwa maelfu ya watu huko Northwest na kuleta theluji kuelekea South na kuzingira Northeast na hali mbaya ya hewa inayolazimisha kuahirishwa kwa mchezo wa NFL, kati ya Pittsburgh Steelers dhidi ya Buffalo Bills ulioandaliwa kufanyika Buffalo, New York.

Forum

XS
SM
MD
LG