Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:43

Papa Francis afuta mkutano Jumatatu kutokana na kusumbuliwa na flu

(FILES) Pope Francis gestures after presiding over a Holy Mass with canonisation ceremony of 18th century missionary Maria Antonia de Paz y Figueroa (1730-1799), also known as "Mama Antula", at the Vatican on February 11, 2024.

Papa Francis amelazimika kufuta  mkutano na waumini  leo Jumatatu asubuhi kwa sababu bado anasumbuliwa na flu, Vatican imesema katika taarifa yake.

Pope Francis akihudhuria ibada ya Jumatano ya Ash huko katika kanisa la Santa Sabina Basilica huko Rome, Italy, February 14, 2024.
Pope Francis akihudhuria ibada ya Jumatano ya Ash huko katika kanisa la Santa Sabina Basilica huko Rome, Italy, February 14, 2024.

Papa huyo mwenye umri wa miaka 87, ambaye alisitisha mikutano yake siku Jumamosi kwa sababu ya mafua, amekumbwa na matatizo ya kiafya mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Alilazimika kufuta safari iliyopangwa ya mkutano wa hali ya hewa wa COP28 huko Dubai mnamo Desemba kwa sababu ya athari za mafua na matatizo katika mapafu.

Hata hivyo Jumapili alitoa ujumbe wake wa kawaida wa Angelus alipotoa wito wa kutatuliwa kwa vita vya Ukraine kwa njia ya kidiplomasia ambayo italeta amani na suluhu ya kudumu.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Forum

XS
SM
MD
LG