Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:05

Papa Francis "achukizwa" na visa vya mimba za kubebewa


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis

Mkuu wa kanisa Katoliki Papa Francis leo Jumatatu ameomba kupigwa marufuku kote ulimwenguni kwa ile alichiokiita visa vya “kuchukiza” vya mimba za kubebewa.

Papa Francis alisema hayo wakti akijumuisha suala la biashara ya ujauzito, kwenye hotuba yake ya kila mwaka, ilioangazia tishio lililopo kwa Amani ya dunia, pamoja na hadhi ya binadamu.

Wakati wa hotuba ya sera za kigeni kwa mabalozi waliopo Vatican, Francis amelalamika kwamba mwaka 2024 umeanza wakati Amani ikiwa imetishiwa, kudhoofishwa au hata katika baadhi ya sehemu, kupotea kabisa. Akiangazia vita vya Russia na Ukraine, Israel na Hamas, uhamiaji, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na utengenezaji haramu wa silaha za nyuklia na silaha zingine hatari.

Aliendelea kuelezea orodha ya baadhi ya mambo yanayoathiri ubinadamu na kuongezeka kwa ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaopelekea hali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG