“Usiku wa leo, mioyo yetu iko Bethlehemu, ambako Mfalme wa Amani kwa mara nyingine tena anakataliwa kufuatia mantiki ya vita, kwa mapambano ya silaha ambayo hata leo inamzuia kupata nafasi duniani”, Papa Francis alisema wakati idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka Gaza.
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameonya Jumapili kwamba vita vya nchi yake dhidi ya Hamas katika eneo hilo vitakuwa vya muda mrefu. “Wacha niweke wazi: Hivi vitakuwa vita vya muda mrefu mpaka Hamas imeondolewa na turejeshe usalama kaskazini na kusini”, Netanyahu alisema katika mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Jumapili.
Wakati mashambulizi ya Israel huko Gaza yakiendelea, zaidi ya Wapalestina 166 waliuawa katika kipindi cha saa 24 zilizopita, na kufanya idadi ya vifo vya Wapalestina kufikia 20,424 kulingana na wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas.
Nayo Israel inasema idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa katika mapigano mwishoni mwa wiki imeongezeka na kufikia 15 na kufikisha idadi ya wanajeshi 161 waliouawa tangu operesheni ya ardhini ya Israel ilipoanza katika Ukanda wa Gaza.
Forum