Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 22:30

Papa Francis asisitiza raia wa maneo ya mizozo waheshimiwe


Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Mungu huko Vatican, Januari 21, 2024
Papa Francis akiongoza sala ya Malaika wa Mungu huko Vatican, Januari 21, 2024

Papa Francis Jumapili amesisitiza raia katika maeneo ya mizozo waheshimiwe na kusema watu wamechoshwa na vita, ambavyo amevitaja kuwa “janga kwa watu na pigo kwa ubinadamu.”

Baada ya sala yake ya kila wiki ya Malaika wa Mungu katika uwanja wa Mtakatifu Petro, Papa amesema misaada ya kibinadamu lazima iruhusiwe kuingia kwa wingi nchini Myanmar na kusema watu lazima waheshimiwe katika eneo la Mashariki ya Kati linalokumbwa na vita kati ya Israel na Hamas.

Ametaja pia mateso ya watu nchini Ukraine.

Jeshi la Myanmar, ambalo liliiondoa madarakani serikali iliyochaguliwa mwaka 2021, limekuwa likipambana na muungano wa majeshi wa makabila ya walio wachache yakipigana ili kumaliza udhibiti wa jeshi katika maeneo yao tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Francis amesema pia alipata taarifa “kwa furaha” kwamba kundi la watu wakiwemo watawa sita, waliachiliwa huru huko Haiti baada ya kushikiliwa mateka kwa karibu wiki nzima.

Wiki iliyopita alikuwa ameomba waachiliwe.

Forum

XS
SM
MD
LG