Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 09:54

Rais wa Argentina akutana na Papa Francis


Rais Javier Milei wa Argentina, na Papa Francis, walikutana kwa mara ya kwanza Jumapili mjini Roma, huku kukiwa na hali mbaya ya kiuchumi katika nchi yao ya asili.

Viongozi hao wawili wenye mitazamo tofauti kuhusu jinsi ya kutokomeza umaskini unaoikumba Argentina, walikutana muda mfupi kabla na baada ya misa ya upapa, wakati wa ziara rasmi ya kwanza ya mchumi huyo mwenye umri wa miaka 53 mjini Roma kama rais wa Argentina.

Milei, mliberali anayeamini soko huria ambaye aliwahi kumwita papa mwenye umri wa miaka 87 kutoka Buenos Aires, mpumbavu ambaye anakuza ukomunisti, alihudhuria sherehe katika kanisa kuu la St Peters kumtawaza mwanamke wa kwanza raia wa Argentina, kuwa mtakatifu.

Kufuatia misa hiyo, Papa Francis, akiwa katika kiti cha magurudumu, alisimama kwa muda ili kupeana mikono na waumini.

Forum

XS
SM
MD
LG