Waziri wa Nishati na pia naibu waziri mkuu Doto Biteko, Jumapili wakati akitembelea kiwanda hicho cha Julius Nyerere chenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 alisema kwamba mtambo uliozinduliwa utaongeza megawati 235 za umeme.
Amesema kwamba uhaba wa umeme ulioshuhudiwa kwa miezi kadha utapungua baada ya kuzinduliwa kwa mtambo wa pili kwenye kiwanda hicho chenye jumla ya mitambo 9, mwezi ujao. Kabla ya kuanza kujengwa kwa mradi huo 2019, wanamazingira walionya kuwa kujengwa kwa bwawa kungeathiri mto muhimu unaopitia kwenye mbuga ya wanyama ya Selous.
Forum