Kuwepo kwa pande zote katika mazungumzo hayo, kila upande ukikutana na wapatanishi katika mji mmoja, kunaamanisha kwamba mazungumzo yamepiga hatua ya kuridhisha kuliko mwanzoni mwa mwezi Februari, ambapo Israel ilitupilia mbali pendekezo la Hamas la sitisho la mapigano kwa kipindi cha miezi minne na nusu.
Rais Joe Biden alisema anatumai sitisho la mapigano litaanza kutekelezwa ndani ya siku chache.
“Natumai ifikapo mwishoni mwa juma hii,”, alisema, alipoulizwa Jumatatu ni lini anatarajia sitisho la mapigano kuanza kutekelezwa.
Biden aliwambia waandishi wa habari wakati wa ziara mjini New York “Mshauri wangu wa usalama wa taifa ameniambia kwamba tunakaribia kufikia makubaliano. Bado hatujamaliza. Matumaini yangu ni kwamba ifikapo Jumatatu ijayo, tutakuwa na sitisho la mapigano.”
Forum