Mashambulizi hayo yalitokea saa tisa alasiri na saa mbili usiku saa za ukanda huo, jeshi la Marekani lilisema, na ni sehemu ya mfululizo wa hatua zilizochukuliwa na Marekani, na washirika wake dhidi ya wanamgambo wa Kiouthi, kwa lengo la kukomesha mashambulizi wanayoyafanya, wakiungwa mkono na Iran.
Mashambulio ya mara kwa mara yamekuwa yakifanywa na wanamgambo hao, kwenye njia za meli za Bahari ya Sham. Mashambulizi hayo matano yalijumuisha kulenga "meli ya Wahouthi isiyo na rubani iliyokuwa chini ya maji, tangu mashambulizi yaanze" mwezi Oktoba, kulingana na taarifa kutoka kwa Kamandi Kuu ya Marekani.
Nyingine kati ya hizo tano lilihusisha chombo kisicho na rubani kilichokuwa kikielea. Matumizi ya vyombo hivyo yamekuwa nadra sana.
Wanamgambo wa Kihouthi, ambao wanadhibiti sehemu kubwa ya Yemen iliyokumbwa na vita, ikiwemo bandari ya Hodeida, walianza mashambulizi yao mwezi Novemba, wakisema walikuwa wanalenga meli zenye uhusiano na Israel, wakiwaunga mkono Wapalestina huko Gaza, ambayo imeharibiwa na vita vya Israel na wanamgambo wa Hamas.
Forum