Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 14:36

Hungary yatarajiwa kuiidhinisha Sweden kujiunga na NATO

Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson, kushoto, akimsikiliza mwenzake wa Hungary, Viktor Orban, wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Carmelite Monastery, Budapest, Hungary, Feb 23, 2024.

Kura ya bunge la Hungary, ambayo inatarajiwa kupitishwa baada ya ziara ya Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson Ijumaa iliyopita - wakati ambapo nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya silaha - itamaliza miezi kadhaa ya uchelewesho wa kukamilisha mabadiliko ya sera ya usalama ya Sweden.

Stockholm iliachana na sera yake ya kutofungamana na upande wowote kwa usalama zaidi ndani ya Shirika la Mkataba wa Atlantiki ya Kaskazini kufuatia uvamizi wa RUSSIA nchini Ukraine mnamo 2022.

Sweden ilitangaza uamuzi wake wakati huo huo na Finland na wakati Finland ikawa mwanachama wa NATO mwaka jana, Sweden ilisubiriwa huku Uturuki na Hungary, ambazo zote zinadumisha uhusiano bora na Russia kuliko wanachama wengine wa muungano unaoongozwa na Marekani, walipinga.

Baada ya Uturuki kuidhinisha uanachama wa Sweden, Taifa la Hungary ndilo lililosalia la mwisho kutoa uamuzi.

Wabunge wa Uturuki wakifuatilia majadiliano ya ombi la Sweden kujiunga na NATO wakiwa katika Bunge la Uturuki, mjini Ankara, Uturuki, Jan. 23, 2024.
Wabunge wa Uturuki wakifuatilia majadiliano ya ombi la Sweden kujiunga na NATO wakiwa katika Bunge la Uturuki, mjini Ankara, Uturuki, Jan. 23, 2024.

Forum

XS
SM
MD
LG