Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Zelenskiy: Ushindi wa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia unategemea msaada wa nchi za Magharibi


Rais wa Ukraine Zelenskiy ashiriki mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa EU na Canada, mjini Kyiv, Februari 24, 2024.
Rais wa Ukraine Zelenskiy ashiriki mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari pamoja na viongozi wa EU na Canada, mjini Kyiv, Februari 24, 2024.

Rais wa Ukraine Volodymr Zelenskiy Jumapili alisema ushindi wa Ukraine katika vita dhidi ya Russia unategemea msaada wa nchi za Magharibi, na kuongeza kuwa ana matumaini washirika wao wa nchi hizo za Magharibi wataipa Kyiv makombora ya masafa marefu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Kyiv, Zelenskiy alisema pia kwamba ana imani kuwa Bunge la Marekani litaidhinisha msaada mpya wa kijeshi na kifedha lakini alibaini kwamba Ukraine inatarajia uamuzi uchukuliwe ndani ya mwezi mmoja.

VOA ilimuuliza Zelenskiy kuhusu uwezekano wa Ukraine kualikwa kwenye mkutano wa NATO unaopangwa kufanyika mjini Washington mwezi Julai.

Alisema “ Ninavyoelewa ni kuwa washirika wote wa NATO wanaunga mkono Ukraine ipewe mwaliko. Na kila mmoja anakubali kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa NATO mnamo siku zijazo. Uamuzi wa kuialika Ukraine unategemea Marekani na Ujerumani. Huu ndio ukweli,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG