Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:08

Ufaransa na Ukraine watasaini mkataba wa pamoja wa usalama Paris Ijumaa


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

Ufaransa na Ukraine zinatarajia kusaini mkataba wa pamoja wa usalama Ijumaa wakati Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiitembelea Paris.

Ofisi ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ilitangaza maendeleo hayo Alhamisi lakini haikutoa maelezo zaidi kuhusu mkataba huo.

Wakati ziara ya Zalenskyy, Macron “atathibitisha tena azma ya Ufaransa kuendelea kutoa msaada usioyumba kwa Ukraine na watu wa Ukraine, kwa kipindi kirefu ikishirikiana na washirika wake wote,” ruais wa Ufaransa ulisema.

Ofisi ya Zelenskyy ilisema pia siku ya Ijumaa atasafiri kwenda Ujerumani kwa mazungumzo na Chansela Olaf Scholz.

Mikutano hiyo inakuja katikati ya mikutano kadhaa ya kimataifa wiki hii, ikiwemo Mkutano wa Usalama wa Munich unaofanyika Jumamosi ambao Zelenskyy anatarajiwa kuhudhuria.

Wakuu wa ulinzi wa NATO walikutana Alhamisi mjini Brussels kujadili jinsi ya kuendeleza msaada wao kwa Ukraine katika mapambano yake dhidi ya uvamizi kamili wa Russia ulioanza takriban miaka miwili iliyopita.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema Alhamisi kuwa washirika watalazimika kuongeza uzalishaji wa vifaa vya ulinzi “kuhakikisha kuwa Ukraine inapata silaha, mahitaji, na risasi na makombora wanayohitaji.”

Stoltenberg alisema kuwa pia anatarajia Bunge la Marekani litakubali kupitisha msaada mpya kwa Ukraine baada ya fedha kumalizika mwezi Desemba.

Mkuu huyo wa NATO aliwaambia waandishi kuwa “kuisaidia Ukraine siyo hatua ya hisani, kuisaidia Ukraine ni uwekezaji kwa usalama wetu.’

Ukraine ilisema Alhamisi wimbi la makombora ya Russia yaliyolenga mikoa kadhaa ya Ukraine, wakati huko katika mji wa Russia wa Belgorod maafisa walisema shambulizi la Ukraine liliuwa watu wasiopungua watano.

Vyacheslav Gladkov, the Belgorod regional governor, said another 18 people were hurt in the Ukrainian attack.

Vyacheslav Gladkov, gavana wa mkoa wa Belgorod, alisema watu wengine 18 walijeruhiwa katika shambulizi lililofanywa na Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Russia imeripoti imetungua roketi 14 katika eneo la Belgorod, ambalo liko karibu na mpaka wa Ukraine na limekuwa eneo la mashambulizi ya mara kwa mara ya Ukraine.

Maafisa wa Ukraine walisema makombora yaliyopigwa na Russia Alhamisi yalijeruhi watu wasiopungua sita na kuharibu majengo kadhaa.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya AP, AFP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG