Wimbi la mashambulizi limekuja wakati mwanadiplomasia wa juu wa EU yuko katika mji mkuu wa Ukraine na Kyiv imewaomba washirika wake wa Magharibi kuongeza misaada ya kijeshi inayohitajika sana, ikiwemo mifumo ya ulinzi wa anga.
Shambulizi katika mji mkuu Kyiv limeua watu wanne wakati jengo refu la makazi ya watu lilipopigwa, na kusababisha moto na kuziathiri ghorofa za juu za jengo hilo kwa moshi mzito.
“Shambulizi jingine dhidi ya nchi yetu,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema katika habari aliyoibandika kwenye mtandao wa kijamii.
"Mashambulizi ya makombora na ndege zisizokuwa na rubani pia yamerikodiwa huko kaskazini mashariki na kusini mwa nchi pamoja na mkoa wa magharibi wa Lviv, mamia ya kilometa kutoka mstari wa mbele.
Forum