Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:19

Mataifa ya Baltic yapongeza juhudi za Marekani za kusaidia Ukraine


Maspika wa mataifa ya Baltic wakizungumza na wanahabari kwenye Ubalozi wa Lithuania mjini Washington. Januari 31, 2024.
Maspika wa mataifa ya Baltic wakizungumza na wanahabari kwenye Ubalozi wa Lithuania mjini Washington. Januari 31, 2024.

Wasemaji kutoka mataifa ya Baltic wameeleza uungaji mkono wao kwa Ukraine dhidi ya uvamizi wa Russia, wakiongeza kuwa msaada wa Marekani kwa Ukraine unashikilia nafasi muhimu kwenye eneo la Indo- Pacific.

Wiki hii maspika wa bunge kutoka Latvia, Lithuania na Estonia wametembelea Washington, ili kufanya mazungumzo na wabunge wa Marekani, akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson, pamoja na maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Marekani.

Johnson kupitia ukurasa wake wa X amesema kwamba walizungumzia changamoto zilizopo, pamoja na umuhimu wa kuzuia vitisho kutoka mataifa kama China, Russia na Iran, wakati wa kikao chao na maspika hao mapema wiki hii.

Mazungumzo hayo yamekuja wakati mjadala kuhusu msaada mpya kwa Ukraine ukiendelea kwenye Baraza la wawakilishi. Ukraine inategemea pakubwa msaada kutoka mataifa ya Magharibi na hasa Marekani, ili kuweza kukabiliana na uvamizi wa Russia, unaokaribia kumaliza miaka miwili tangu ulipoanza.

“Inaonekana kwamba Russia inajiandaa kwenye vita vya muda mrefu, “amesema Lauri Hussar ambaye ni Spika wa Bunge la Estonia.

Forum

XS
SM
MD
LG