Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 03:55

Ukraine yadai kuharibu meli ya kijeshi ya Russia


Meli ya kijeshi ya Russia kwa jina Caesar Kunikov, inayodaiwa kushambuliwa na Ukraine.
Meli ya kijeshi ya Russia kwa jina Caesar Kunikov, inayodaiwa kushambuliwa na Ukraine.

Jeshi la Ukraine limesema Jumatano kwamba limeharibu meli ya kijeshi ya Russia yenye uwezo wa kutua ndege kwenye bahari ya Black Sea, karibu na eneo lililokaliwa na Russia la Crimea.

Jeshi hilo limetambulisha meli hiyo kama Caesar Kunikov, likiongeza kuwa ilikuwa kwenye maji karibu na mji wa Alupka, wakati iliposhambuliwa. Kufikia sasa hakuna ripoti yoyote kutoka upande wa Russia kuhusiana na tukio hilo.

Vikosi vya Ukraine vimeharibu meli kadhaa za Russia kwenye bahari ya Black Sea tangu Russia ilipofanya uvamizi halisi dhidi ya Ukraine karibu miaka miwili iliopita. Wizara ya Ulinzi ya Russia imeripoti kuwa mfumo wake wa ulinzi wa anga umeharibu droni 9 za Ukraine usiku kucha, zikiwemo 6 kwenye bahari ya Black Sea.

Droni nyingine 2 zilinaswa kwenye anga ya Belgorod, wakati nyingine moja ikiharibiwa kwenye eneo la Voronezh, wizara hiyo imeongeza. Mafisa wa Ukraine kwa upande wao wameongeza kusema kwamba mashambulizi kadhaa usiku kucha yameua takriban watu 3 karibu na mji wa mashariki mwa Ukraine wa Donetsk.

Forum

XS
SM
MD
LG