Mfumo wa ulinzi wa anga wa Ukraine umeangusha droni 14 kati ya hizo , ambazo ni aina ya Shahed kutoka Iran, ikiwa ni moja wapo ya silaha zinazotumiwa. Silaha hizo zimenaswa kwenye maeneo tofauti ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Khemelnytskyi, Vinnystia, Kirovohrad, Mykolaiv, Dnipro-petrovsk, na Zaporizhzhia.
Mykhailo Fedorov, waziri wa masuala ya dijitali wa Ukraine ameambia Reuters kwamba Ukraine inapanga kutengeneza maelfu ya droni zake za masafa marefu mwaka huu, zenye uwezo wa kufanya mashambulizi ndani ya Russia.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy Jumapili usiku wakati wa hotuba yake ya kila siku kwa taifa amesema kwamba Ukraine inajitahidi kuimarisha mfumo wake wa ulinzi wa anga, pamoja na ule wa kielektroniki, kama vipaumbele vya mwaka huu kwenye vita vyake dhidi ya Russia.
Forum