Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:08

Seneti ya Marekani yapitisha mswada wa kuzisaidia Ukraine, Israel na Taiwan


Kiongozi wa walio wachache kwenye Baraza la Senate la Marekani, Mitch McConnell,
Kiongozi wa walio wachache kwenye Baraza la Senate la Marekani, Mitch McConnell,

Baraza la Seneti la Marekani Jumanne limepitisha mswada kwa ajili ya msaada wa Ukraine, Israel na Taiwan wenye thamani ya karibu  dola bilioni 95.34, lakini kungali na wasi wasi ikiwa utaidhinishwa na baraza la wawakilishi linaloshikiliwa na Warepublican.

Mswada huo umeishinishwa baada ya miezi kadhaa migumu ya mashauriano na kujitokeza kwa mgawanyiko wa kisiasa ndani ya chama cha Republican, kuhusu jukumu la Marekani nje ya nchi.

Uwamuzi ulifikiwa baada ya kundi dogo la warepublican waliokua wanapinga msaada wa dola bilioni 60 kwa ajili ya Ukraine, kubadili msimamo kufuatia majadiliano ya muda mrefu usiku, wakitumia saa za mwisho kubishana kama Marekani izingatie zaidi matatizo yake yenyewe, kabla ya kutuma fedha zaidi nje ya nchi.

Lakini zaidi ya darzeni za warepublican walipiga kura na karibu wademokrati wote walipitisha kwa kura 70-29 huku wafuasi wakibishana kwamba kutelekeza Ukraine kunaweza kuongeza nguvu kwa rais wa Russia Vladmir Putin na kutishia usalama wa taifa kote katika kanda hiyo.

Kiongozi wa walio wengi wa baraza la seneti Chuck Schumer, anayefanya kazi kwa karibu na kiongozi wa republican Mitch McConell kuhusu sheria amesema imekuwa miaka au miongo mingi tangu seneti

Forum

XS
SM
MD
LG