Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:40

NATO kutoa euro bilioni 100 kwa Ukraine


Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO.
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO wamejadili jinsi ya kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine kwa muda mrefu leo Jumatano.

Katika mkutano wao lilikuwepo pendekezo la kutoa Euro bilioni 100 (dola bilioni 107) ufadhili wa miaka mitano, mpango ambao unaonekana kuwa utaisadia Kyiv.

Mapendekezo ya Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg yataupa muungano huo wa Magharibi nafasi ya moja kwa moja katika kuratibu usambazaji wa silaha na vifaa kwa Ukraine huku ikipambana na uvamizi wa Russia, wanadiplomasia wanasema.

Mipango hiyo itajadiliwa wakati wa mkutano wa siku mbili mjini Brussels ambao utaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Mkataba wa North Atlantic na kujiandaa kwa mkutano wa kilele wa Julai wa viongozi wa muungano huko Washington.

Forum

XS
SM
MD
LG