Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:54

Poland yaitaka Russia kueleza ukiukaji mpya wa anga

Kundi la wakimbizi katika kituo cha ununuzi cha Tesco, kilicho kati ya mji wa mpaka wa Medyka, na Przemysl, Poland, Machi 4, 2022 (Picha ya AP/Marc Sanye)
Kundi la wakimbizi katika kituo cha ununuzi cha Tesco, kilicho kati ya mji wa mpaka wa Medyka, na Przemysl, Poland, Machi 4, 2022 (Picha ya AP/Marc Sanye)

Poland ilisema Jumapili kwamba itaitaka Russia kueleza ukiukaji mpya wa anga baada ya kombora la Russia kuingia kwenye  anga ya  nchi hiyo  ya NATO kwa takriban kilomita 2 Jumapili asubuhi kabla ya kurejea Ukraine, kulingana na msemaji wa jeshi la Poland.

Anga ya Poland iliingiliwa na mojawapo ya makombora yaliyorushwa usiku na vikosi vya anga vya serikali ya shirikisho la Russia, jeshi lilisema kwenye mtandao wa X, na kuongeza, kuwa chombo hicho kiliruka kwenye anga ya Poland juu ya kijiji cha Oserdow katika mkoa wa Lublin) na kukaa kwa sekunde 39.

Zaidi ya yote, tunawataka Russia kukomesha mashambulizi yake ya anga ya kigaidi dhidi ya wakazi na eneo la Ukraine, kumaliza vita na kuzingatia matatizo ya ndani ya nchi yao msemaji wa wizara ya mambo ya nje Pawel Wronski alisema, kwa mujibu na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG