Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 13:57

Mahakama ya Tunisia yatoa hukumu ya kifo kwa wauwaji wa mwanasiasa mashuhuri


Wakili na kiongozi wa upinzani wa Tunisia, Chokri Belaid, aliyeuwawa 2013.
Wakili na kiongozi wa upinzani wa Tunisia, Chokri Belaid, aliyeuwawa 2013.

Mahakama moja ya Tunisia Jumatano imetoa hukumu ya kifo kwa watu wanne, na wengine wawili wamehukumiwa kifungo cha maisha, baada ya kukutwa  na hatia ya kumuua mwanasiasa mashuhuri Chokri Belaid miaka 11 iliyopita, yakiwa  mauaji ya kwanza ya kisiasa nchini humo ndani ya miongo kadhaa.

Belaid ambaye alikuwa mwanasiasa wa mrengo wa kushoto alikuwa mkosoaji mkali wa chama cha Islamic Ennahda, akidai kuwa hakikuwa kikichukua hatua dhidi ya ukatili uliokuwa ukitekelezwa na watu wenye misimamo mikali dhidi ya wale wenye misimamo ya wastani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiongozi huyo alipigwa risasi Februari, 6, 2013, wakati kifo chake kikilishtua taifa na kupelekea maandamano makubwa. Tukio hilo lilifanyika wakati taifa likiwa tayari limekumbwa na mapinduzi ya kiarabu ya 2011, ambapo maandamano yalianza Tunisia na kisha kuingia kwenye mataifa mengine, na kuwaondoa madarakani viongozi kadhaa wa kidikteta wa muda mrefu.

Forum

XS
SM
MD
LG