Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:54

Kiwanda cha Dangote kutishia biashara ya mafuta ya Ulaya


Picha ya sehemu ya kiwanda cha kusafishia mafuta cha Dangote karibu na mji Lagos, Nigeria.
Picha ya sehemu ya kiwanda cha kusafishia mafuta cha Dangote karibu na mji Lagos, Nigeria.

Kiwanda cha kusafisa mafuta cha Dangote huenda kikafikisha kikomo biashara ya mafuta ya miaka mingi kutoka Ulaya hadi Afrika, yenye thamani ya dola bilioni 17 kila mwaka, huku viwanda wa Ulaya vikiwa kwenye hatari ya kufungwa kutokana na ushindani mkubwa uliopo, wachambuzi wanasema.

Kiwanda cha Dangote kilianza shuguli zake Januari kiligharimu dola bilioni 20 kujenga. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha mapipa 650,000 kwa siku, na kitakuwa kikubwa zaidi barani Afrika na Ulaya, pindi kitakapofikia kilele chake cha usafishaji kufikia mwaka ujao.

Kiwanda hicho kimetajwa kuwa ukurasa mpya kwenye sekta ya nishati ya Nigeria, wakati taifa hilo linaloongoza kwa wingi wa watu barani Afrika, likijitahidi kupata uhuru wake kwenye sekta hiyo. Takriban thuluthi moja ya mapipa milioni 1.33 kwa siku ya mafuta kutoka Ulaya mwaka uliopita yalipelekwa kwenye mataifa ya Afrika magharibi, kikiwa kiwango kikubwa zaidi ya eneo lolote lingine.

Forum

XS
SM
MD
LG