Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:56

Waisraeli wanaopinga serikali waandamana nje ya bunge mjini Jerusalem


Maandamano Israeli
Maandamano Israeli

Darzani za maelfu ya Waisraeli Jumapili walikusanyika nje ya jengo la bunge mjini Jerusalem katika maandamano makubwa Zaidi ya kuipinga serikali tangu nchi hiyo ilipoingia vitani mwezi Oktoba mwaka jana.

Wanaitaka serikali kufikia makubaliano ya kuwaachilia huru dazani za mateka wanaoshikiliwa na wanamgambo wa Hamas huko Gaza, na kufanya uchaguzi wa mapema.

Takriban miezi sita ya vita imefichua mgawanyiko mpya katika jumuiya ya Waisraeli.

Wakati Hamas imepata hasara kubwa, bado iko nguvu, na familia za mateka zinaamini kuwa, kadri muda unavyosonga, ndivyo maisha ya mateka hao yanazidi kuwa hatarini.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anasema kuitisha uchaguzi mpya kabla ya ushindi huko Gaza, kutalemaza uwezo wa Israeli, kwa muda wa miezi sita hadi minane, na kuzuia mazungumzo kuhusu kuachiliwa kwa mateka.

Forum

XS
SM
MD
LG