Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:24

Mahakama ya Umoja wa mataifa yaamuru Israel kufungua njia zaidi kwa misaada ya Wapalestina


Mahakama ya Kimataifa ya sheria ikisikiliza kesi kuhusu athari za kisheria kwa Israel kukalia maeneo ya Wapalestina, Februari 21, 2024. Picha ya Reuters
Mahakama ya Kimataifa ya sheria ikisikiliza kesi kuhusu athari za kisheria kwa Israel kukalia maeneo ya Wapalestina, Februari 21, 2024. Picha ya Reuters

Mahakama ya juu ya Umoja wa mataifa Alhamisi iliamuru Israel kufungua njia zaidi za ardhini kuelekea Gaza ili kuruhusu misaada zaidi ya kibinadamu kwa Wapalestina wenye njaa kuingia kwenye eneo hilo.

Amri hiyo ya Mahakama ya Kimataifa ya sheria mjini the Hague, ambayo inaiwajibisha Israeli kisheria, iliitaka nchi hiyo kuchukua “ hatua zote zinazohitajika na zenye ufanisi kuhakikisha bila kupoteza muda” kwamba huduma za msingi na msaada wa kibinadamu unapelekwa huko,” ikiwemo chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu.

Mahakama hiyo iliamuru pia Israel kuhakikisha mara moja “kwamba jeshi lake halitekelezi tena vitendo ambavyo ni ukiukaji wa haki yoyote ya Wapalestina huko Gaza kama kundi la watu wanaolindwa chini ya mkataba kuhusu kuzuia na kuadhibu uhalifu wa mauaji ya kimbari, ikiwemo kuzuia, kupitia hatua yoyote, utoaji wa msaada wa dharura wa kibinadamu.”

Mahakama imeiomba Israel kutoa ripoti ndani ya mwezi mmoja kuhusu jinsi ilivyotekeleza amri hizo.

Israel haikutoa mara moja maelezo juu ya uamuzi huo, lakini ilikanusha vikali kufanya mauaji ya kimbari katika mwenendo wake katika vita vya karibu miezi sita dhidi ya wanamgambo wa Hamas. Iliitaka Mahakama hiyo ya Umoja wa mataifa kutotoa amri mpya.

Forum

XS
SM
MD
LG