Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 15:00

Mamlaka ya Palestina imetangaza kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri


Rais wa Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas

Rais Mahmoud Abbas alimteua Mohammad Mustafa, mshauri wa muda mrefu kuwa Waziri Mkuu wa Palestina mapema mwezi huu.

Mamlaka ya Palestina imetangaza kuundwa kwa baraza jipya la mawaziri wakati ikikabiliwa na shinikizo la kimataifa la kufanya mageuzi.

Rais Mahmoud Abbas ambaye ameongoza chama cha PA kwa karibu miongo miwili na bado anaudhibiti wa jumla alitangaza serikali mpya katika amri ya rais leo Alhamisi. Hakuna hata mmoja wa mawaziri wanaoingia ni mtu anayejulikana. Abbas alimteua Mohammad Mustafa, mshauri wa muda mrefu, kuwa Waziri Mkuu mapema mwezi huu.

Mustafa, mwanasiasa huru ambaye ni mchumi aliyesomea Marekani aliapa kuunda serikali ya kiteknolojia na kuunda mfuko huru wa fedha ili kusaidia kuijenga tena Gaza. PA inasimamia sehemu za Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu na Israeli. Vikosi vyake vilifurushwa kutoka Gaza wakati Hamas ilipotwaa madaraka mwaka 2007 na haina nguvu huko.

Marekani inatoa wito wa kuundwa upya kwa PA ili kusimamia Gaza baada ya vita na hatimaye kuelekea kutambulika kwa taifa huru. Israel inakataa wazo hilo, ikisema itadumisha udhibiti wa usalama wa wazi katika Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG