Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 01:38

China yaunga mkono rasimu ya UN ya sitisho la mapigano Gaza


Lin Jian
Lin Jian

China ilisema Jumatatu inaunga mkono rasimu ya azimio jipya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu sitisho la “haraka"  la mapigano huko Gaza, baada ya taifa hilo na Russia kupinga azimio la awali lililopendekezwa na Marekani.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Lin Jian alisema . China inaunga mkono rasimu ya azimio hili na inaipongeza Algeria na nchi nyingine za Kiarabu kwa bidii yao katika suala hili.

Vita hivyo vilianza na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la Hamas mnamo Oktoba 7 ambalo lilisababisha takriban vifo 1,160 nchini Israel, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya AFP iliyotokana na takwimu rasmi za Israeli.

Israel imeapa kuwaangamiza wanamgambo hao, ambao pia waliwakamata mateka wapatao 250, ambapo Israel inaamini kuwa takriban 130 wamesalia Gaza, wakiwemo 33 wanaodhaniwa kuuawa.

Wizara ya afya katika Ukanda wa Gaza inayoendeshwa na Hamas siku ya Jumapili iliweka idadi ya vifo katika eneo hilo kufikia 32,226, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.

Baraza hilo limegawanyika kuhusu vita vya Israel na Hamas tangu mashambulizi ya Oktoba 7, na kuidhinisha maazimio mawili tu kati ya manane, huku yote mawili yakihusu misaada ya kibinadamu kwa eneo lililoharibiwa la Ukanda wa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG