Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:20

Kiongozi wa Wademocrat katika Baraza la Seneti Marekani aomba uchaguzi mpya nchini Israel


Kiongozi wa walio wengi katika Seneti ya Marekani, Chuck Schumer
Kiongozi wa walio wengi katika Seneti ya Marekani, Chuck Schumer

US SCHUMER-ISRAEL Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti la Marekani Chuck Schumer, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu Myahudi nchini Marekani, Alhamisi alitoa wito kwa Israel kuitisha uchaguzi mpya.

Schumer, mshirika wa muda mrefu wa Israel, alisema Netanyahu kuna hatari akaifanya nchi yake kuchukuliwa kama “mkandamizaji mkubwa wa haki” katika masuala ya dunia.

Tangu Hamas ilipoua watu 1,200 katika shambulio baya la Oktoba 7 na kuwashikilia mateka watu 240, mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel yameua zaidi ya Wapalestina 31,000 huko Gaza, kulingana na wizara ya afya chini ya utawala wa Hamas.

Schumer, kiongozi wa Wademocrat katika Baraa la Seneti, alisema Israel katika mashambulizi yake ya anga na ardhini kwenye eneo dogo kando na Bahari ya Mediterranean “ yamekuwa mabaya mno kuweza kuvumilia mateso ya raia huko Gaza, na kusababisha uungwaji mkono kwa Israel duniani kote kudorora sana.

Alisema wananchi wa Israel wamechoshwa na msimamo wa utawala uliokwama katika fikra za zamani.

“Kama taifa la kidemokrasia, Israel ina haki ya kuchagua viongozi wake, na tunapaswa kuwaacha watu wajiamulie mustakabali wao,” Schumer alisema.

“Lakini jambo muhimu ni kwamba Waisrael wanapewa fursa ya kuamua. Kuna umuhimu wa kuwa na mjadala mpya kuhusu mustakabali wa Israel baada ya shambulio la Oktoba 7.”

“Kwa maoni yangu, hilo linawezekana kwa kuitisha uchaguzi,” alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG