Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:09

Shirika la Hilali Nyekundu Palestina lasema watano wauwawa wakati wa utoaji wa misaada Jumamosi huko Gaza


 Malori ya Hilali Nyekundu ya Misri yakiwa yamepakia foleni ya misaada nje ya mpaka wa Rafah na Ukanda wa Gaza wa Palestina Machi 23, 2024, huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas.
Malori ya Hilali Nyekundu ya Misri yakiwa yamepakia foleni ya misaada nje ya mpaka wa Rafah na Ukanda wa Gaza wa Palestina Machi 23, 2024, huku kukiwa na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas.

Shirika la Hilali Nyekundu la Palestina limesema watu watano waliuwawa na darzeni  wengine kujeruhiwa kwa risasi na mkanyagano wakati wa utoaji wa misaada Jumamosi huko Gaza, ambapo njaa inakaribia.

Video za AFP zimeonyesha msafara wa malori yakipita kwa haraka kwenye vifusi vinavyoungua karibu na eneo la usambazaji wakati wa giza la alfajiri huku watu wakipiga kelele na milio ya risasi baadhi yao ikiwa ni milio ya risasi za maonyo, mashahidi walisema.

Shirika la Hilali Nyekundu lilisema ilitokea baada ya maelfu ya watu kukusanyika kwa ajili ya kuwasili kwa takriban lori 15 za unga na vyakula vingine, ambavyo vilipaswa kugawiwa katika mzunguko wa Kuwait wa Jiji la Gaza, kaskazini mwa eneo hilo.

Mzunguko huo umekuwa eneo la matukio kadhaa ya machafuko na mauti kutokana na usambazaji wa misaada, ikiwa ni pamoja na moja la Machi 23 ambapo serikali inayoongozwa na Hamas ilisema watu 21 waliuwawa na mashambulizi ya Israeli mashtaka ambayo Israeli ilikanusha.

Forum

XS
SM
MD
LG