Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 05:23

Senegal:Kiongozi wa upinzani na mwenzake mgombea wa urais waachiliwa huru kutoka jela


Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko

Kiongozi wa upinzani mwenye ushawishi mkubwa nchini Senegal Ousamne Sonko na mgombea wa urais anayeunga mkono katika uchaguzi wa Machi 24, Bassirou Diomaye Faye, waliachiwa huru kutoka jela Alhamisi, televisheni ya serikali ya Senegal RTS ilisema kwenye tovuti yake.

Kuachiliwa kwao kulikuwa kunatarajiwa kufuatia sheria ya msamaha iliyopitishwa na bunge tarehe 6 Machi, huku viongozi wakijaribu kupunguza mvutano baada ya mpango wao wa kuahirisha uchaguzi kwa miezi 10 kukwama.

RTS haikutoa maelezo zaidi, na haikufahamika mara moja wawili hao walielekea wapi baada ya kuachiliwa.

Maelfu ya wafuasi walikusanyika barabarani anakoishi Sonko mjini Dakar, wakiimba jina lake na kucheza huku wakishikilia mabango yenye picha yake.

Sonko alitoa wito kwa wafuasi wake kumuunga mkono Faye katika kinyang’anyiro cha urais, tishio kwa washindani wake kwa sababu Sonko ana uungwaji mkono mkubwa, hasa miongoni mwa vijana waliokatishwa tamaa na matatizo ya kiuchumi na ukosefu wa ajira katika taifa hilo la Afrika Magharibi lenye watu milioni 17.

Forum

XS
SM
MD
LG