Nyumba ya Mapisa-Nqakula ilivamiwa mwezi uliopita na wapelelezi, ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa rushwa, hata ingawa hawakutoa maelezo kuhusu uchunguzi huo wala madai hayo.
"Kujiuzulu kwangu sio dalili au kukubali hatia kuhusiana na tuhuma zinazotolewa dhidi yangu," alisema katika taarifa.
Kujiuzulu huko, ambako kunaanza kutekelezwa mara moja, pia kunaambatana naye kuacha kazi kama mbunge.
Mapisa-Nqakula alikuwa waziri wa ulinzi kutoka 2012 hadi 2021. Shirika la utangazaji la serikali ya Afrika Kusini SABC liliripoti kwamba anashukiwa kupokea mamilioni ya pesa taslimu kama hongo kutoka kwa mwanakandarasi wa zamani wa kijeshi.
Mapisa-Nqakula alichukua likizo maalum baada ya uvamizi huo, na Jumanne, ombi lake kwa mahakama kuzuia mamlaka kumkamata, lilitupiliwa mbali.
Forum