Familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza na Hamas siku ya Jumanne walimkashifu kiongozi wa nchi yao huku hasira dhidi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alivyoshughulikia vita hivyo ikiongezeka katika usiku wa nne mfululizo wa maandamano makubwa.
Maelfu ya watu walikusanyika mbele ya bunge la nchi hiyo, huku familia za mateka na waziri mkuu wa zamani Ehud Barak akimlaumu Netanyahu kwa "maafa" ya Oktoba 7 na kutaka uchaguzi ufanyike.
Katika maandamano ya Jumanne mbele ya bunge, baadhi ya familia zilimshutumu kiongozi wa muda mrefu zaidi wa Israel kwa kujaribu kutumia vita hivyo kuongeza muda wake wa kutawala.
Waandamanaji walikabilian na vikosi vya usalama vilivyojaribu kuwazuia kusonga mbele karibu na makazi ya Netanyahu huku wengine wakikamatwa.
Forum