Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 19:42

Blinken anaelekea Ufaransa na Ubelgiji kujadili hali ya Gaza, Haiti na Ukraine


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akiwa mjini Washington, DC. March 25, 2024. (Photo by Mandel NGAN / AFP)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken akiwa mjini Washington, DC. March 25, 2024. (Photo by Mandel NGAN / AFP)

Blinken anaanza ziara yake mjini Paris, ambako wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema atakutana na Rais Emmanuel Macron

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anasafiri wiki hii kwenda Ufaransa na Ubelgiji kwa mazungumzo mapana ambayo yanajumuisha majadiliano juu ya hali nchini Ukraine, Gaza na Haiti pamoja na mazungumzo ya kibiashara na Umoja wa Ulaya na Armenia.

Blinken anaanza ziara yake mjini Paris, ambako wizara ya mambo ya nje ya Marekani inasema atakutana na Rais Emmanuel Macron kuhusu kuiunga mkono Ukraine, kuzuia vita vya Israel na Hamas huko Gaza na kuleta utulivu nchini Haiti.

Marekani na Ufaransa zimekuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa Ukraine katika kipindi cha miaka miwili tangu Russia ilipoanzisha uvamizi wa jirani yake. Blinken pia anatarajiwa kuelezea uungaji mkono wa Marekani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni wakati akifanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay.

Forum

XS
SM
MD
LG