Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 16:22

Jeshi la israel limesema vikosi vyake viliondoka hospitali ya Shifa


Muonekano wa jengo la hospitali ya Shifa huko Gaza City. March 28, 2024. (Photo by AFP)
Muonekano wa jengo la hospitali ya Shifa huko Gaza City. March 28, 2024. (Photo by AFP)

Jeshi la Israel limesema limewaua wanamgambo 200 katika eneo la hospitali hiyo ya Shifa

Jeshi la Israel limesema Jumatatu kuwa vikosi vyake viliondoka katika eneo la hospitali ya Shifa kaskazini mwa Gaza baada ya kukamilisha operesheni huko.

Kuondoka kwa wanajeshi kunajiri wiki mbili baada ya vikosi vya Israel kuanzisha operesheni hiyo katika hospitali kubwa zaidi ya Gaza, wakiwashutumu makamanda wa Hamas kwa kutumia eneo hilo kufanya operesheni za kigaidi.

Jeshi la Israel limesema limewaua wanamgambo 200 katika eneo la hospitali hiyo, ambako lilitekeleza mapigano ya ardhini na mashambulizi ya anga.

Miili ilipatikana ndani na nje ya jengo la hospitali wakati watu waliporejea katika eneo hilo kufuatia kuondoka kwa vifaru na wanajeshi wa Israel.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Jumapili kuwa ameidhinisha mpango wa operesheni za kijeshi katika mji wa Rafa kusini mwa Gaza, eneo ambalo limezua wasiwasi wa kimataifa wakati nusu ya wakaazi wa Gaza wanapata hifadhi huko kutokana na vita.

Forum

XS
SM
MD
LG