Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 01:49

Wafanyakazi 7 wa misaada wauliwa kwenye shambulizi la anga la Israel huko Gaza


Mtu akikagua gari ambalo wafanyakazi wa misaada wa World Central Kitchen waliuawa ndani ya Gaza. Aprili 2. 2024
Mtu akikagua gari ambalo wafanyakazi wa misaada wa World Central Kitchen waliuawa ndani ya Gaza. Aprili 2. 2024

Kundi la Misaada la World Central Kitchen, WCK, limesema Jumanne kwamba shambulizi la anga la Israel limeuwa wafanyakazi wake 7 huko Gaza, na hivyo linasitisha mara moja shughuli zake katika eneo hilo.

WCK katika taarifa limesema kwamba limekamilisha ufikishaji wa tani 100 za msaada wa chakula kwenye ghala moja mjini Deir al Balah, na kwamba msafara wa magari mawili ya kivita yenye nembo yake ulikuwa ukiondoka mjini humo wakati shambulizi lilipotokea. Limesema kuwa shambulizi hilo la anga limefanyika licha ya kuwepo mawasiliano na jeshi la Israel.

Miongoni mwa waliokufa ni pamoja na raia mmoja wa Palestina, raia wa Australia, Poland, Uingereza na Mmarekani mwenye asili ya Canada, shirika hilo limesema. Mtendaji mkuu wa WCK, Erin Gore, aliliita shambulizi hilo kama lisilowezai kusamehewa.

“Hili silo tu shambulizi dhidi ya WCK pekee, ni shambulizi dhidi ya mashirika yote ya kibinadamu yanayopeleka misaada, kwenye eneo ambako chakula kinatumiwa kama silaha ya vita,” ameongeza Gore. Mwanzilishi wa shirika hilo Jose Andres kupitia kwenye mitandao ya kijamii “amevunjika moyo na kuomboleza kutokana na vifo vya dada yetu na kaka zetu kutokana na shambulizi la IDF huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG