World central kitchen moja kati ya mashirika mawili yasio ya kiserikali yanayofanya juhudi kubwa kupeleka msaada wa chakula kwa kutumia boti imesema Jumanne kwamba “shambulizi lililolengwa na Israel “ Jumatatu limeuwa wafanyakazi wa msaada wa Australia, Uingereza, Palestina, Poland, Marekani na Canada.
Washington ambayo ni mshirika mkubwa wa Isarel imesema imevunjika moyo sana na kusumbuliwa na shambulizi hilo.
Waziri mkuu wa uingereza Rishi Sunak amesema Jumannekuwa amesikitishwa na shambulizi hilo la mauaji ya wafanyakazi wa msaada wa World central kitchen na ametoa rambirambi zake na kutoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina wa tukio hili la kusikitisha.
"nimeshtuka na kusikitishwa kusikia ripoti za vifo vya wafanyakazi wa msaada Gaza. Wanafanya kazi nzuri sana, kupunguza mateso ambayo wengi wanapata huko Gaza, wanapaswa kusifiwa na kupongezwa kwa kile wanachokifanya," alisema waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.
"Wanahitaji kuruhusiwa kufanya kazi hiyo bila kuzuiliwa, na ni wajibu wa Israel kuhakikisha kwamba wanaweza kufanya hivyo na tunaiomba Israel kufanya uchunguzi wa kilichotokea haraka, kwa sababu ni wazi kuna maswali tunayohitaji kujibiwa.” aliongeza.
Wakati huohuo waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema shambulizi hilo limetekelezwa na israel bila kukusudiwa.
Forum