Wabunge ambao kwa idadi kubwa walipititisha sheria ambayo itaongeza ufuatiliaji wa haki za mashoga katika taifa hilo la Afrika Magharibi wamekuwa wakimtaka Akufo-Addo atangaze sheria hiyo mpya.
Lakini ofisi ya rais imesema hautaupeleka mswaada huo kwa rais kuidhinishwa mpaka mashitaka hayo mawili dhidi yasuluhishwe, yamezua ukosoaji bungeni.
Mbunge mmoja wa upinzani, Rockson-Nelson Dafeamekpor, aliwasilisha uchelewesho huo mahakama kuu, ambayo imetoa hukumu dhidi ya malalamiko yake siku ya Jumatatu.
Jaji Lordina Serwaa Mireku amesema mahakama imefanya uamuzi haitakuwa sahihi kumlazimisha Akufo-Addo kushughulikia sheria ambayo inapambana na changamoto mbili za kisheria katika mahakama kuu.
Mwanasheria wa Dafeamekpor amesema atakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Watu wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Ghana tayari wanakabiliwa adhabu ya kifungo cha hadi miaka mitatu jela.
Iwapo sheria hiyo itaanza kufanya kazi, itaongeza muda wa kifungo jela na ufutiaji wa haki za mashoga na wanatuhumiwa kuukukuza utambulisho wa mashoga, wasagaji na makundi mengine ya watu wachache au utambulisho wa kijinsia.
Forum