Uamuzi huo unaweza ukachangia kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya mashoga kote barani Afrika, ikiwa ni pamoja na nchini Ghana ambapo wabunge pia walipitisha sheria dhidi ya mashoga mwezi Februari. Pia inaweza kuwa na athari za kiuchumi kwa nchini hiyo ya Afrika Mashariki, muuzaji nje mkuu wa kahawa katika bara la Afrika.
Kupitishwa kwa sheria ya kupinga mapenzi ya watu wa jinsia moja nchini Uganda mwezi Mei mwaka jana, kulizua vikwazo mbalimbali kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, vikiwemo kutoka Benki ya Dunia na Marekani.
Benki ya Dunia ilisitisha utoaji wa mikopo mipya kwa nchi hiyo huku Marekani ikitangaza tahadhari za usafiri.
Chini ya sheria ya AHA vitendo vya jinsia moja na shughuli zinazohusiana navyo, huvutia adhabu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kifo kwa kosa la ulawiti uliokithiri, huku mapenzi ya jinsia moja yakivutia kifungo cha maisha.
Uamuzi huo unatarajiwa saa nne asubuhi , saa za Afrika Mashariki, mmoja wa mawakili wa walalamishi Nicholas Opiyo, aliandika kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Forum