Mwanamke na mwanaharakati aliyejibadilisha jinsia yake, Angel Maxine alikimbilia Berlin kabla ya bunge kupitisha mswaada wa dhidi ya LGBTQ akihofia usalama wa marafiki ambao amelazimika kuwaacha.
Jumatano wabunge kwa kauli moja walipitisha sheria itakayoongeza ukandamizaji dhidi ya mashoga na wale wanaoshutumiwa kuhamasisha ushoga au utambulisho mwingine wa aina hiyo katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
Tayari kulikuwa na adhabu ya hadi kifungo cha miaka mitatu jela kwa wale wanaojihusisha na ushoga nchini Ghana. mswaada huo uliokuwa sheria unaweka adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela kuhamasisha, kufadhili, na kusaidia shughuli za ushoga.
Mtafiti wa Amnesty international wa Afrika Magharibi Michele Eken amesema mswaada huo unakiuka haki za msingi,
“Unapuoangalia mswaada huo nchini Ghana, unakiuka haki za msingi ambazo Ghana inazilinda kwa mujibu wa katiba pamoja na haki za binadamu za kimataifa. Alisema Eken
“Una haki ya kuheshimu utu wa kibinadamu, ambao ni msingi katika katiba ambayo itakuwa imekiukwa. Haki ya faragha, haki ya uhuru wa kujieleza, haki ya kukusanyika. Watu hawawezi kuzungumza wazi na watu wanaweza kuteswa na kulengwa kwa kuzungumza kwa uhuru.” Aliongeza
Wakati wabunge wanasema tabia ya utetezi wa mashoga inakiuka maadili ya utamaduni wa Ghana.
Forum