Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 22:58

Mahakama ya Uganda kusikiliza keshi iliyowasilishwa na jamii ya LQBTQ


Mwanaume akiwa na kibango kinachotetea haki ya mashoga Uganda. Picha ya maktaba. Machi 25, 2023.
Mwanaume akiwa na kibango kinachotetea haki ya mashoga Uganda. Picha ya maktaba. Machi 25, 2023.

Mahakama nchini Uganda leo Jumatatu imeanza kusikiliza kesi inayopinga sheria kali iliyopitishwa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, inayotaoa hukumu ya kifo kwa baadhi ya matendo ya wapenzi hao, pamoja na hukumu ya  kifungo cha miaka 20 jela kwa kuendeleza ushoga.

Sheria hiyo maarufu kama Anti Homosexuality Act, AHA, ilitiwa saini na rais Yoweri Museveni mwezi Mei, hatua iliyopelekea Marekani na Benki ya Dunia kuiwekea Uganda vikwazo.

Kupitia kikao cha muda mfupi, jopo la majaji watano litatathimini malalamiko yaliyowasilishwa kwa maandishi, wakati kiongozi wa jopo hilo Richard Buteera akisema kwamba waliowasilisha wanatafahamishwa pale uamuzi utakapotolewa.

Nicholas Opiyo ambaye ni wakili wao amesema kwamba wanatumai mahakama itachukua muda wake kueleza iwapo katiba ya Uganda inalinda haki za kila mmoja kwenye jamii, bila kubagua aina ya mapenzi wanayozingatia.

Forum

XS
SM
MD
LG