Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:06

Idadi ya raia wanaokufa yaongezeka wakati Israel ikizidisha mashambulizi Gaza


Timu ya Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina likiwafikisha waliouawa katika hospitali ya Al-Awda, huko Jabalia, Ukanda wa Gaza.
Timu ya Shirika la Mwezi Mwekundu la Palestina likiwafikisha waliouawa katika hospitali ya Al-Awda, huko Jabalia, Ukanda wa Gaza.

Idadi ya Raia wanaokufa  inaendelea kuongezeka wakati Israel ikiwa imezidisha  mashambulizi upande wa kaskazini na kusini mwa Gaza siku ya Jumatatu.

Timu ya waokoaji waliwaleta raia waliojeruhiwa vibaya sana, baadhi yao ni watoto, katika hospitali iliyoko kaskazini mwa Beit Lahiya.

Baadhi ya mapigano makali sana ya wiki kadhaa yanaendelea kote upande wa kaskazini na kusini.

Majeshi ya Israeli yalikuwa yamerejea Jabalia, ambapo wamesema wameweza kuivunja Hamas miezi kadhaa iliyopita, ili kuwazuia wanamgambo hao kujikusanya huko.

Mfanyakazi wa afya, Fares Afana, anasema wamejaribu kuifikia kambi ya Jabalia.

Miili iligunduliwa huko baada ya mashambulizi ya usiku kucha.

Lakini anadai kuwa majeshi ya Israeli yalikuwa yanalenga wafanyakazi wa magari ya kubeba wagonjwa, wakiwazuia kuwaokoa raia waliojeruhiwa na waliokwama.

Upande wa kusini mwa Gaza, huko Rafah, mitaa yote ilikuwa mitupu huku Wapalestina wakiwa wamekimbia mapigano.

Israel Jumatatu ilifunga barabara kuu inayoingia Rafah, na kufunga kivuko kikuu cha kupitisha misaada.

Umoja wa Mataifa unasema mfanyakazi wa kigeni wa usalama aliuwawa Jumatatu wakati gari iliyokuwa na nembo ya UN ikielekea hospitali huko Rafah iliposhambuliwa.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa kifo cha mfanyakazi wa kimataifa wa UN huko Gaza ambako vita inaendelea.

Kitengo cha kijeshi cha Hamas kinasema kutokana na mashambulizi ya mabomu yanayofanywa na Israeli imepoteza mawasiliano na wanamgambo waliokuwa wanawalinda mateka wanne wa Israeli, akiwemo Hersh Goldberg-Polin mwenye uraia pacha wa Marekani na Israeli, ambaye alikuwa ameonekana katika kanda ya video iliyotolewa na Hamas mwezi Aprili.

Vita kati ya Israel na Hamas vilianza baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.

Forum

XS
SM
MD
LG