Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:46

Mashambulizi yanayofanywa na Israel yaitikisa Gaza, vita kuhamia Rafah


TOPSHOT - Watoto wakishuhudia moshi ukipaa angani wakati Israel ikifanya mashambulizi ya angani mashariki mwa Rafah eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza Mei 13, 2024, wakati vita kati ya Israel na Hamas vikiendelea. (Photo by AFP)
TOPSHOT - Watoto wakishuhudia moshi ukipaa angani wakati Israel ikifanya mashambulizi ya angani mashariki mwa Rafah eneo la kusini mwa Ukanda wa Gaza Mei 13, 2024, wakati vita kati ya Israel na Hamas vikiendelea. (Photo by AFP)

Milipuko mikubwa ya mabomu inayotokana na mashambulizi ya anga na mizinga iliyorushwa iliutikisa upande wa kaskazini mwa Gaza kuanzia Jumamosi (Mei 11), moshi uliokuwa ukitoka katika  majengo ulionekana kutoka Israel huku mapigano kati ya Israel na Hamas yakiendelea.

Jeshi la Israel lilisema limewataka wakaazi na watu wasiokuwa na makazi katika eneo la Jabalia la kaskazini mwa Gaza kuondoka, linasema linarejea operesheni yake huko baada ya kutambua Hamas wanajaribu kujiimarisha ili walidhibiti eneo hilo.

Israel pia ilisema imewataka Wapalestina katika maeneo mengine kusini mwa Gaza katika mji wa Rafah kuondoka na kuelekea kwa kile walichokiita eneo lililopanuliwa la kibinadamu huko Al-Mawasi, ikiwa ni ishara kwamba jeshi hilo linashinikiza kuendelea na mipango yake ya mashambulizi ya ardhini huko Rafah.

Wizara ya Afya ya Palestina ilisema Wapalestina wasiopungua 37, 24 kati yao ni kutoka eneo la kati la Gaza, waliuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanyika usiku kucha katika eneo hilo finyu, ikiwemo Rafah, mji wa upande wa kusini zaidi wa Ukanda huo unaopakana na Misri. Haitofautishi ni watu wangapi kati yao ni raia au wanamgambo.

Jeshi la Israeli lilisema ndege yake ilipiga malengo kumi eneo la Gaza katika siku iliyopita, ikiongeza majeshi yake ya ardhini yalikuwa yametokomeza wapiganaji takriban 30 huko Zeitoun.

Vita kati ya Israel na Hamas vilianza baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.⁣ -

Forum

XS
SM
MD
LG