Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:49

UNRWA inasema wakimbizi 80,000 wameukimbia mji wa Rafah huko Gaza


Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina-UNRWA
Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina-UNRWA

Madhara kwa familia hizi hayavumiliki. Hakuna mahali salama, UNRWA ilisema kwenye mtandao wa X.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA, limesema Alhamisi kuwa takriban watu 80,000 wameukimbia mji wa Rafah tangu Jumatatu wakati Israel ilipozidisha operesheni zake katika eneo la kusini mwa Gaza City.

Madhara kwa familia hizi hayavumiliki. Hakuna mahali salama, UNRWA ilisema kwenye mtandao wa X. Waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz amesema jeshi la nchi yake litaendelea kupambana na Hamas hadi pale litakapowa-angamiza.

Matamshi yake yamekuja siku moja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kusema Marekani haitatoa silaha za mapigano kwa Israel kwa ajili ya matumizi huko Rafah, huku pia ikielezea nia yake ya dhati kuilinda Israel.

Hatua hiyo imefuatia wiki kadhaa za maafisa wa Marekani kuelezea kupinga mipango ya Israel ya kufanya mashambulizi katika eneo la Rafah, huku maafisa wa Israel wakieleza umuhimu wa kufanya operesheni huko ili kufikia malengo ya kuwashinda Hamas na kuwaachia huru mateka waliokuwa wakishikiliwa Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG