Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 07:12

Kwa nini Marekani imeamua kusitisha usafirishaji wa baadhi ya shehena za silaha kwenda Israel?


(FILES) Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kushoto, akisalimiana na Rais wa Marekani Joe Biden wakati alipowasili Tel Aviv October 18, 2023.
(FILES) Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kushoto, akisalimiana na Rais wa Marekani Joe Biden wakati alipowasili Tel Aviv October 18, 2023.

Huku Marekani hivi karibuni iliamua kusitisha usafirishaji wa baadhi ya shehena kwa Israel, vita huko Gaza sasa vimekuwa ni sehemu ya mjadala mkali sana kuhusu kampeni ya Rais wa Marekani.

Donald Trump amejiunga na Warepublican wengine katika kumkosoa hasimu wake wa kisiasa, Rais Joe Biden, kwa msimamo wa Biden kwa suala hilo. Veronica Balderas Iglesias anaripoti.

Rais wa zamani Donald Trump akiwa mahakama ya uhalifu Manhattan huko New York City, Mei 10, 2024.
Rais wa zamani Donald Trump akiwa mahakama ya uhalifu Manhattan huko New York City, Mei 10, 2024.

Ilikuwa ni Jumapili ya majonzi nchini Israel wakati ikiadhimisha Siku ya Kumbukumbu kwa wanajeshi waliofariki na waathirika wa vitisho.

Upande mwingine wa mpaka, Wapalestina wasiokuwa na makazi walitekeleza amri iliyotolewa ya kuondoka kabla ya mpango wa Israel wa kupanua operesheni zake za kijeshi dhidi ya Hamas huko Rafah, katika mji wa kusini huko Gaza.

Kinachotokea upande mwingine wa dunia pia kinasikika kwa nguvu sana kwenye kampeni hapa Marekani. Mgombea urais wa Republican Donald Trump amezungumzia vita vya Israel na Hamas wakati alipohutubia umati wa takriba wafuasi wake laki moja siku ya Jumamosi huko Wildwood, New Jersey.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema:“Huenda kusingekuwa na vita huko Gaza na sisi White House. Wakati nilipokuwa rais, tulikuwa na amani Mashariki ya Kati kuliko hapo kabla.”

Trump na Warepublican wengine wamekashifu vikali…. uamuzi wa karibuni wa utawala wa Biden wa kusitisha upelekaji wa shehena ya mabomu huko Israel.

..kutokana na matukio yanayotokea huko Rafah.

Seneta Mrepublican Lindsey Graham ameuelezea ukosoaji wake Jumapili katika muktadha wa Vita vya Pili vya Dunia.

Lindsey Graham
Lindsey Graham

Seneta Lindsey Graham, Mrepublican anasema: “Wakati tulipokabiliwa na uharibifu kwama taifa baada ya Pearl Harbor, mapigano ya Wajerumani na Wajapani, tuliamua kumaliza vita kwa kuipiga bomu Hiroshima na Nagasaki kwa kutumia silaha za nyuklia. Huo ulikuwa uamuzi sahihi. Wape Israel mabomu wanayohitaji kumaliza vita ambavyo hawawezi kumudu kushindwa, na kufanya kazi ya kupungua maafa.”

Lakini hata baadhi ya shehena za silaha zimesimamishwa, ripoti ya karibuni ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa Bunge ilishindwa kuhitimisha kwamba Israel imekiuka sheria za Marekani na Kimataifa wakati walipotumia msaada wa kijeshi wakati wa vita dhidi ya Hamas.

Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken aliulizwa kwenye kituo cha televisheni cha NBC kama Marekani inakwepa kumwajibisha mshirika wake.

Antony Blinken
Antony Blinken

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje, Marekani anaeleza: “Hapana, msimamo tofauti. Tuaitendea Israel kama moja ya washirika wetu na marafiki wa karibu kama tutakavyoitetea nchi nyingine yoyote. Na tunapofikia hitimisho la uhakika, sisi, ingawaje litakuwa gumu sana litakuwa ni katikati ya vita.”

Seneta Bernie Sanders anayejitegemea na mpenda maendeleo, ambaye anaelemea upinzani wa Democratic kwa vitendo vya Israel katika vita, amekiambia kituo cha televisheni cha NBC kwamba kwa maoni yake, Israel isipatiwe hata senti moja la msaada wa kijeshi wa Marekani

Seneta Bernie Sanders, Mdemocrat asema: “….Wapalestina 35,000 wamefariki na 77,000 wamejeruhiwa, theluthi mbili kati ya hao ni wanawake na watoto. Hiyo si njia ya kuendesha vita katika jamii iliyostaarabika kwa kiwango ambacho vita hivyo ni vya kistaarabu.”

Ilitarajiwa kwamba Joe Biden, ambaye hadi hivi sasa ameweza kuweka uwiano kati ya juhudi zake ya kuchaguliwa kwake tena na majukumu yake rasmi kama rais, atakabiliwa na changamoto mpya wiki hii kutoka kwa Warepublican katika bunge juu ya kusitisha baadhi ya misaada ya kijeshi kwa Israel.

Donald Trump, wakati huo huo, atarejea mahakamani Jumatatu na kukabiliana na mfanyakazi wake wa zamani, Michael Cohen, wakati Cohen atapotoa ushahidi katika kesi inayomkabili Trump huko New York ya kulipa pesa ili kuficha mahusiano yake.

Forum

XS
SM
MD
LG