Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:24

Jeshi la Israel limesema vikosi vyake vimechukua udhibiti Rafah


Vikosi vya Israeli vimefanya operesheni ya angani na ardhini katika sehemu za mashariki mwa Rafah
Vikosi vya Israeli vimefanya operesheni ya angani na ardhini katika sehemu za mashariki mwa Rafah

Israel inasema mashambulizi katika eneo la Rafah yalikuwa muhimu kufikia lengo lao la kuwashinda Hamas

Jeshi la Israel limesema leo Jumanne vikosi vyake vimechukua udhibiti wa Gaza upande wa Rafah kwenye kivuko kati ya Ukanda wa Gaza na Misri, siku moja baada ya kuwaamuru maelfu ya Wapalestina kuondoka katika eneo hilo na kufanya mashambulizi ya anga ya mara kwa mara.

Operesheni hiyo ya Israel inakuja baada ya wiki kadhaa za maafisa wa Israel kusema mashambulizi katika eneo la Rafah yalikuwa muhimu ili kufikia lengo lao la kuwashinda Hamas, wakati Marekani, Umoja wa Mataifa na mataifa mengine yakionya kuwa kuanzisha mashambulizi katika eneo lililojaa raia wa Palestina huenda ikasababisha maafa ya kibinadamu.

Nina hofu kwamba hali hii itasababisha vifo vingi, vifo vya raia. Vyovyote wanavyosema, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aliwaambia waandishi wa habari leo Jumanne. Hakuna maeneo salama huko Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG