Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 19:28

Jeshi la Israel linajianda kufanya mashambulizi ya ardhini huko Rafah


Kambi inayowahifadhi Wapalestina waliohamishwa kwenye makazi yao na mashambulizi ya Israel inaonekana huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, Februari 27, 2024. Picha ya AP
Kambi inayowahifadhi Wapalestina waliohamishwa kwenye makazi yao na mashambulizi ya Israel inaonekana huko Rafah, katika Ukanda wa Gaza, Februari 27, 2024. Picha ya AP

Jeshi la Israel Jumatatu limesema watu katika maeneo ya mashariki mwa mji wa Rafah wanapaswa kuelekea kwenye eneo ambalo jeshi limeliita eneo kubwa la kibinadamu ambalo linajumuisha Khan Younis, katika hatua ambayo inajiri kabla ya shambulizi lililopangwa la Israel huko Rafah.

Msemaji wa jeshi la IDF akiandika kwenye mtandao wa kijamii kwa Kiarabu, amesema jeshi la Israel litachukua hatua kali dhidi ya taasisi za kigaidi huko Rafah, na kwamba yeyote ambaye yuko katika eneo hilo atakuwa ameyaweka maisha yake hatarini.

Israel inaandaa “operesheni ya wigo mdogo” huko Rafah, msemaji wa jeshi amesema, na inakadiriwa watu 100,000 ndio wameombwa kuondoka katika eneo la uokoaji.

Awali Israel ilitoa onyo kama hilo wakati wa kampeni yake ya kulitokomeza kundi la wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza. Wapalestina wengi mjini Rafah walikwenda huko kutafuta hifadhi baada ya Israel kuwaonya kukimbia maeneo mengine ya Gaza.

Forum

XS
SM
MD
LG