Ni moja ya mashambulio mabaya kufanyika hadi sasa katika mkoa wa Belgorod, Ukraine ilifanya kile maafisa wa Russia wamesema ilikuwa shambulio kubwa la makombora na mifumo ya roketi.
Picha kutoka eneo la tukio zimeonyesha ghorofa 10 za jengo hilo zikiporomoka. Baadaye, wakati wafanyakazi wa huduma za dharura walipokuwa wanafukua vifusi kuwatafuta manusura, paa liliporomoka na watu wakakimbia ili kunusuru maisha yao, vumbi na vifusi vikianguka nyuma yao.
Wizara ya ulinzi ya Russia imesema shambulio hilo ambalo imeliita “la kigaidi” kwenye makazi ya watu, lilifanyika nyakati za asubuhi na kulirushwa takriban makombora 12.
Forum