Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 00:58

Kuvurugika kwa misafara ya meli za kimatiafa za mizigo kwaongezeka


FILE PHOTO: Meli ya mizigo ya kikundi cha usafirishaji cha Maersk.
FILE PHOTO: Meli ya mizigo ya kikundi cha usafirishaji cha Maersk.

Kuvurugika kwa misafara ya meli za mizigo katika Bahari ya Sham kumeongezeka na inatarajiwa kupunguza uwezo wa sekta hiyo kati ya nchi za Mashariki ya Mbali na Ulaya kwa kiasi cha asilimia 15 -20 katika robo ya pili ya mwaka, kikundi cha usafirishaji cha Maersk kilisema Jumatatu.

Maersk na kampuni nyingine kadhaa zimebadilisha safari zake na kuzungukia Afrika katika Cape of Good Hope tangu mwezi Disemba kuepuka mashambulizi ya wanamgambo wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran katika Bahari ya Sham, ambapo safari ndefu zimesababisha gharama za usafirishaji mizigo kupanda zaidi.

“Eneo la hatari limeongezeka, na mashambulizi yanaenea nje ya eneo la pwani,” Maersk ilisema katika ilani mpya iliyotoa kwa wateja wake Jumatatu.

“Hii imevilazimisha vyombo vyetu kufanya safari ndefu zaidi, ikipelekea ongezeko la muda na gharama ya kufikisha mizigo yako katika nchi inakopelekwa kwa wakati huu,” iliongeza taarifa hiyo.

Kampuni ya Denmark, inayoangaliwa kama kipimo cha biashara ya kimataifa, wiki iliyopita ilisema kuwa safari za meli zimekabiliwa na misukusuko iliyosababishwa na mashambulizi yanayofanyika katika Bahari ya Sham yanatarajiwa kuendelea kwa kukadiria hadi kufikia mwisho wa mwaka.

Forum

XS
SM
MD
LG