Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:25

Jeshi la Marekani ladai kudungua ndege za Wahouthi kwenye bahari ya Shamu


Wafuasi wa wa-Houthi wakiwa kwenye maandamano ya kukemea Marekani mjini Sanaa, Yemen, Feb. 23, 2024.
Wafuasi wa wa-Houthi wakiwa kwenye maandamano ya kukemea Marekani mjini Sanaa, Yemen, Feb. 23, 2024.

Jeshi la Marekani pamoja na washirika wake limesema kwamba limedungua droni 15 zilizorushwa na Wahouthi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran kwenye bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden Jumamosi.

Muda mfupi baadaye waasi wa Kihouthi walidai kurusha silaha dhidi ya meli ya mizigo ya Marekani kwenye bahari ya Shamu, kama kampeni ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa wanamgambo wa Hamas wanaoungwa mkono na Iran huko Gaza, ambako Israel inaendelea na mashambulizi.

Kamandi ya kijeshi ya Marekani ya CENTCOM, imesema kwamba mashambulizi hayo makali kutoka kwa Wahouthi yamefanyika kabla ya kupambazuka, kwenye bahari ya Shamu na Ghuba ya Aden. Desemba, Marekani ilitangaza operesheni ya kijeshi ya kulinda meli za mizigo kwenye bahari ya Shamu kutokana na mshambulizi ya wa-Houthi, ambayo yamelazimisha baadhi ya meli kutumia njia mbadala.

Mauaji ya kwanza kutokana na mshambulizi hayo yameripotiwa wiki hii, wakati serikali ya Ufilipino ikisema kwamba wafanyakazi wake wawili ni miongoni mwa watu waliokufa kwenye shambulizi dhidi ya meli ya mizigo ya True Confidence.

Forum

XS
SM
MD
LG